Viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, walipofika nyumbani kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, kumfariji kufuatia msiba wa kuondokewa na Mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.
Viongozi wengine walioambatana na Mhe. Waziri Prof. Shemdoe kumfariji Mheshimiwa Rais ni Naibu Katibu Mkuu OWM–TAMISEMI, Bw. Sospeter Mtwale, na Naibu Katibu Mkuu OWM–TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila.
Katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI inamtakia Mheshimiwa Rais afya njema, subira, faraja na utulivu, na inawatakia wafiwa wote moyo wa kustahimili majonzi ya kumpoteza mpendwa wao

