Dar es Salaam. Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sokabet imetumia jumla ya Sh44, 658,787,637 kuwazawasia washindi mbalimbali kwa mwezi Agosti.

Hayo yalisemwa na Meneja Msaidizi wa Huduma kwa Wateja wa Sokabet Tanzania, Lazaro Mduma, wakati wa wa zoezi la kumkabidhi fedha mmoja wa washindi, Alisema R. Likwawa ambaye alishindi Sh Sh143.1 milioni kuoitia mchezo wa Shining Crown

Mduma alisema kuwa Likwawa ni moja ya washindi walishinda fedha nyingi katika michezo yao mbalimbali na kushika nafasi ya pili huku A. Mwakalinga akishika nafasi ya kwanza kwa kupata Sh180 milioni.

Mwakalinga alishinda fedha hizo kupitia mchezo wa slot wa mtandaoni unaofahamika kama 20 Burning Hot unaotolewa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sokabet Tanzania.

Mduma alisema kuwa nafasi ya tatu imechukuliwa na B. Mushi akipata Sh109m katika mchezo wa 40 Extra Crown Buy Bonus huku F. Mwasumbi alishinda Sh98.48 milioni na E. Kessy alipata Sh82.8 milioni kwa mchezo wa 40 Super Hot.

Washindi wengine ni H. Omary aliyepata Sh80 milioni, G. Nkya Sh50.3 milioni, M. Mbwambo Sh24.2 milioni na E. Shirima aliyeshinda Sh24 milioni Walishinda kupitia mchezo wa Live Casino Crazy Time

Pia katika orodha hiyo ni Asha Kimaro alijinyakulia Sh21.53 milioni, D. Massawe akipata Sh21.29 milioni na N. Mgaya alipata Sh20 milioni katika mchezo wa Monopoly. Washindi wengine waliotajwa katika matokeo hayo ni H. Chande aliyeshinda Sh19.6 milioni, G. Mwakasege Sh18.76 milioni na K. Lyimo Sh17.34 milioni.

Mduma alisema Sokabet Tanzania inatoa michezo ya slot mtandaoni katika makundi mbalimbali, yakiwamo video slots, classic slots, jackpot, free spins na michezo yenye chaguo la kununua bonansi ambapo wateja wanaweza pia kutumia huduma ya USSD kwa kubonyeza *149*35#, www.sokabet.co.tz au kupiga simu 0800 784242 kwa maelezo Zaidi

“Mbali na michezo ya slot, jukwaa hilo pia linatoa huduma za Live Casino, Virtual Games, Crash Games na sports na bidhaa nyingine za michezo ya mtandaoni,” alisema. Pia Sokabet inamchezo wa Zeppelin ambao wenye mfanano na aviator ambao umetoa zaidi ya kiasi 3,837,558,164 kwa mwezi agosti.

Kwa upande wake, Mwakalinga alisema amefurahishwa na ushindi huo mkubwa, akisema hakutarajia kupata kiasi hicho cha fedha.

“Nina furaha sana kushinda kiasi hiki cha fedha. Sikuwa na fikra za siku moja kupata ushindi huu mnono kwa kutumia kiasi kidogo tu katika kucheza michezo ya mtandaoni ya kampuni ya Sokabet,” alisema.

Alisema anapanga kutumia kwanza kukaa na familia yake wapange kwa pamoja sehemu ya fedha hizo katika uwekezaji ili kuboresha maisha yake na ya familia yao kwa ujumla.

“Nitatumia fedha hizo kwa kufanya mambo mbaimbali ya maendeleo yangu na familia yangu. Nawashauri vijana wenye umri zaidi ya miaka 18 kuendelea kubashiri na Sokabet ambao wana michezo mbalimbali ya mitandaoni ambayo inakupa chaguo kubwa katika kucheza,” alisema.