Hafla ya uzinduzi wa majengo ya Wizara, taasisi za Serikali na barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, iliyokuwa ifanyike kesho Septemba 8, 2026, imeahirishwa.
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) imesema tarehe mpya ya uzinduzi huo itatangazwa baadaye.
