Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Makamu wa Rais,
Samuel Mwashambwa
*********************
Ofisi ya Makamu wa Rais imeshiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma yaliyoanza Juni 16 hadi Juni 23 mwaka huu kwa kutoa elimu kwa
wananchi na kushiriki shughuli za kijamii.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Makamu wa Rais,
Samuel Mwashambwa amesema shughuli mbalimbali za kutoa elimu kuhusu
masuala ya Muungano na Mazingira zimeanza kufanyika kupitia vyombo vya
habari.
Mwashambwa alisema tathmini ya kampeni ya marufuku ya mifuko ya plastiki na
masuala yanayotakiwa kufanyika baada ya hatua hiyo pamoja na kuendeleza
kampeni ya matumizi ya mifuko mbadala imeanza kufanyika.
Aliongeza kuwa wananchi wataelimishwa kuhusu aina za mifuko mbadala yenye
ubora unaotakiwa kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa miongozo.
"Katika kwenda sambamba na sera ya viwanda wananchi watapata wasaa wa
kufahamu tathmini ya athari kwa mazingira ili kuhakikisha Tanzania ya viwanda
inafanikiwa na pia wataelimishwa kuhusu wajibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais
katika matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa pamoja na bidhaa au viumbe
watokanao na teknolojia hii," alisema.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi huyo, Wiki ya Utumishi wa Umma itatumika
katika kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya Muungano kwa ujumla
ikiwemo mafanikio katika kuondoa changamoto zake.
Maadhimisho haya ni kwa mujibu wa kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo
nchi wanachama huadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu
Utumishi wa Umma hivyo aliwataka wananchi waendelee kufuatilia vyombo
mbalimbali vya habai kupata elimu.
Kwa mwaka huu kauli mbiu ni Uhusiano kati ya Uwezeshaji wa Vijana na
Usimamizi wa Masuala ya Uhamiaji; Kujemga Utamadni wa Utawala Bora,
Matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utaoaji Huudma Jumuishi.