Mkuu wa Idara ya Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Yvonne Maruma akizungumza katika Wiki ya Ubunifu Tanzania 2026 ambapo alizungumzia namna ya Vodacom inavyounganisha Watanzania na kuleta tija kupitia Zaidi ya Mtandao: Hususani Watengeneza maudhui na Majukwaa Mtandaoni kwa kuwapa mtandao bora na simu janja zinazo unga mkono ubunifu wao.
Mkuu wa Idara ya Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Yvonn Maruma (kulia) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango Dr. Blandina Kilama baada ya kumaliza majadiliano ya namna ya kuziunganisha sauti za Watanzania: Watengeneza maudhui na Majukwaa Mtandaoni. Tukio hilo limefanyika katika Wiki ya Ubunifu Tanzania leo hii.
Mkuu wa Idara ya Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Yvonne Maruma (kulia) akisalimiana na Mhariri Mtendaji mkuu wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited baada ya kumaliza majadiliano ya namna ya kuziunganisha sauti za Watanzania: Watengeneza maudhui na Majukwaa Mtandaoni. Tukio hilo lilifanyika katika Wiki ya Ubunifu Tanzania leo hii.
Mkuu wa Idara ya Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Yvonne Maruma (wa pili kushoto), akisikiliza majadiliano yaliyohusu namna ya kuziunganisha sauti za Watanzania: Watengeneza maudhui na Majukwaa Mtandaoni. Tukio hilo lilifanyika wakatib wa Wiki ya Ubunifu Tanzania.
Mkuu wa Idara ya Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Yvonne Maruma (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited Rosalynn Mndolwa-Mworia (wa pili wa kushoto), Meneja wa Uchunguzi wa Vodacom Tanzania Joseph Mnyune (kushoto) na Meneja Biashara Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communication Limited Tess Aloyce (wa pili kulia) wakizungumza wakati wa Wiki ya Ubunifu Tanzania ambapo Vodacom Tanzania walishiriki katika majadiliano ya namna ya kuziunganisha sauti za Watanzania: Watengeneza maudhui na Majukwaa Mtandaoni. Tukio hilo lilifanyika katika Wiki ya Ubunifu Tanzania leo hii.
……………
Ni katika Wiki ya Ubunifu Tanzania (IWTz) 2026
Katika Wiki ya Ubunifu Tanzania (IWTz) 2026, Vodacom Tanzania imeonyesha mchango wa mtandao, ubunifu na ujasiriamali katika kufanikisha Dira ya Maendeleo Tanzania 2050. Tukio hilo limewakutanisha wabunifu, wajasiriamali, watunga sera, wawekezaji, vijana na wadau mbalimbali chini ya kauli mbiu: “Kutoka Matarajio hadi Mageuzi: Kuibua Njia ya Tanzania Kuelekea Ustawi Jumuishi.”
Vodacom imeshiriki katika mjadala kuhusu uchumi wa watengeneza maudhui, maonesho, mikutano na wadau na shughuli za kuelimisha kuhusu usalama wa mtandao.
Akizungumza katika mjadala wa watengeneza maudhui na majukwaa mtandaoni, Mkuu wa Idara ya Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Yvonne Maruma, alisema mtandao una thamani zaidi kupitia fursa unazowawezesha Watanzania kuzipata katika elimu, biashara na ubunifu.
Kupitia Vodacom Youth Base (VYB), kampuni inaendelea kuwawezesha watengeneza maudhui kubaki mtandaoni na kukuza shughuli zao za kidijitali. Ushiriki wa Vodacom katika IWTz 2026 unaunga mkono malengo ya Dira ya Maendeleo 2050 kupitia mageuzi ya kidijitali, uvumbuzi na ukuaji wa uchumi jumuishi.
