Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga SC, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliopigwa leo mjini Tanga.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Albert Kangwanda, Max Nzengeli, Mudathir Yahya pamoja na Zimbwe Jr, huku bao la kufutia machozi la Coastal Union likifungwa na Gradi Kiala.
Kufuatia matokeo hayo, Yanga SC imefikisha pointi sita baada ya kushinda michezo miwili, na imepanda kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikimshusha Simba SC.
Yanga SC na Simba SC zina pointi sawa, lakini Yanga inaongoza kutokana na kuwa na tofauti nzuri zaidi ya mabao.
