Afisa Masoko wa chuo hicho ,Lilian Mollel akizungumza katika.mahafali hayo ya 17 jijini Arusha
Na Happy Lazaro, Arusha.
ZAIDI ya Wahitimu Elfu saba katika.fani mbalimbali za ufundi na ujuzi wameweza kuhitimu katika chuo cha Eureka Driving school na Eureka Collage tangu kuanzishwa kwa chuo hicho na kuweza kuondokana na changamoto ya soko la ajira kwa kujiajiri wenyewe.
Aidha chuo hicho kimefanya mahafali yake ya 17 tangu kuanzishwa kwake ambapo mpaka sasa zaidi ya wahitimu elfu saba wameweza kuhitimu katika fani mbalimbali za ufundi na ujuzi zinazowawezesha kujiajiri na kuajiriwa tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.
Akizungumza katika mahafali hayo Afisa Masoko wa chuo hicho ,Lilian Mollel amesema kuwa ,chuo hicho kimeendelea kutoa mchango mkubwa katika kuwaandaa vijana wenye maarifa na stadi zinazokidhi mahitaji ya soko la ajira.
“Eureka ni miongoni mwa vyuo vyenye historia ndefu katika utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya vitendo ambapo kwa miaka mingi, kimeendelea kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea kupitia mafunzo yanayolenga ajira na ujasiriamali.”amesema Lilian.
Amesema kuwa ,chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali zikiwemo ususi na urembo, udereva wa magari katika madaraja ya Basic, PSV na HGV, Tour Guiding, Hotel Management pamoja na kozi nyingine za ujuzi zinazowaandaa wanafunzi kwa maisha ya kazi na biashara.
Aidha Lilian amewahimiza wazazi na walezi kuwapeleka vijana wao chuo cha Eureka ili wapate elimu ya vitendo itakayowasaidia kujiajiri badala ya kusubiri ajira za kuajiriwa ambapo chuo hicho kimeweka mkazo katika kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuanzisha shughuli zao mara baada ya kuhitimu.
“Kwa mwaka huu, Eureka College kimefanikiwa kuhitimisha idadi kubwa ya wanafunzi, huku wengi wao tayari wakianza kujiajiri katika sekta mbalimbali, ikiwemo huduma za kompyuta, stationery na biashara nyingine ndogo zinazotumia ujuzi walioupata chuoni.”amesema Lilian.
Amefafanua kuwa,chuo hicho kitaendelea kuboresha ubora wa mafunzo na kupanua kozi zake ili kuzalisha wahitimu wenye uwezo wa kushindana katika soko la ajira na kuchangia maendeleo ya Taifa kupitia elimu ya ufundi na ujuzi.
Naye mgenirasmi katika mahafali hayo Katibu Tawala msaidizi anayehusika na viwanda,biashara na uwekezaji mkoa wa Arusha ,Frank Mmbando amekipongeza chuo hicho kwa kuendelea kutoa watalaamu wazuri waliobobea katika fani mbalimbali huku wakiwaandaa kuweza kujiajiri.
Mmbando amewataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata chuoni hapo kuweza kujiajiri na kuweza kuondokana na changamoto ya ajira
