…………………………………………………………………………………………..
Katika kuelekea sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limejipanga kikamilifu kuhakikisha wakazi wa Mkoa wa Mbeya, wageni na wakazi wa mikoa jirani wanasherehekea sikukuu hii kwa amani na utulivu.
Kwa kutambua kuwa Mkoa wetu unapakana na nchi jirani ya Malawi pia barabara kuu inayounganisha nchi yetu na nchi jirani pamoja na mikoa jirani imepita hapa, tumejipanga vizuri kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa barabara wakiwemo madereva na watembea kwa miguu. Wito wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ni kwa watumiaji wote wa barabara kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Sambamba na hilo, tumejipanga vizuri kuhakikisha maeneo yeto tete kama vile Mlima Nyoka, Mlima Iwambi, Mlima Igawilo na Mwansekwa ulinzi na usalama umeimarishwa katika kipindi chote cha sikukuu ya Pasaka kama ilivyo kwa siku nyingine.
Kuelekea kipindi hiki cha sikukuu, waumini wa madhehebu ya Kikristu ushiriki katika ibada/misa kwa nyakati tofauti kulingana na ratiba zao, Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha ulinzi na usalama katika makanisa hasa katika misa au ibada za mkesha ikiwa ni pamoja na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya COVID 19 kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na viongozi wa kitaifa pamoja na wataalamu wa Wizara ya Afya.
Kuelekea msimu huu wa sikukuu ya Pasaka, ni wito wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia ulinzi na usalama wa mtoto, kuhakikisha wanakaa na watoto nyumbani ili pia kujiepusha na matembezi yasiyokuwa ya lazima.
Pia tunasitiza ulinzi na usalama katika makazi yetu, kuhakikisha kwa wale wanaotoka kwenda katika misa au ibada za mkesha kuacha waangalizi pia kuhakikisha tunajilinda kwa kufunga milango na madirisha ili kuepuka uhalifu katika nyumba zetu.
Sambamba na hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limepiga marufuku Disco Toto na Madisco mengine ambayo kwa namna moja au nyingine yatapelekea mikusanyiko ya watu. Kamanda MATEI amesisitiza hilo wakati akiongea na waandishi wa Habari na kusema, “Jeshi la Polisi halijapokea ombi wala kutoa kibali cha mtu kufanya Disco au shughuli yoyote itakayopelekea mkusanyiko wa watu” Hivyo amewataka wananchi na wakazi wa Mkoa wa Mbeya kukaa nyumbani na kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na viongozi wa Serikali Kuu na Wizara ya Afya dhidi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona – COVID 19.
Aidha Jeshi la Polisi linaendelea kusisitiza utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu kupitia namba za simu za viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kama ifuatavyo:-
RPC……………………………………………………………..0715 009 931
RCO [Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa]………0658 376 052
STAFF OFFICER [Msaidizi wa RPC]………………….……0658 376 006
OPERATION OFFICER [Mkuu wa Operesheni Mkoa]..…..0754 466 924
RTO [Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa]……0658 376 472
OCD MBEYA………………………………………………….0659 884 996
OCD MBALIZI………………………………………………..0655 248 381
OCD CHUNYA………………………………………………..0782 746 543
OCD MBARALI……………………………………………….0659 885 948
OCD RUNGWE……………………………………………….0659 885 253
OCD KYELA………………………………………………….0659 887 919