Timu ya Taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa England mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa nchini Marekani.

Kutokana na ushindi huo, Argentina itamenyana na Hispania katika fainali ya Kombe la Dunia 2026, huku England ikivaana na Ufaransa katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.