Timu ya Taifa ya Hispania imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Ufaransa katika mchezo wa nusu fainali.
Kufuatia ushindi huo, Hispania itamkabili mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Argentina na England, mchezo utakaochezwa kesho kuanzia saa 4:00 usiku.
Kwa upande wa Ufaransa, itacheza mechi ya kuwania nafasi ya tatu dhidi ya timu itakayopoteza nusu fainali ya pili kati ya Argentina na England.
Mabao ya Hispania katika mchezo huo yalifungwa na Mikel Oyarzabal na Pedro Porro.
