KITETO – Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mhe. Edward Ole Lekaita, na Mbunge wa Jimbo la Kilindi, Mhe. Salehe Mbwana Mhando, wameahidi kushirikiana kuhakikisha barabara ya Lengatei–Songe inajengwa kwa kiwango cha changarawe ili iweze kupitika kwa mwaka mzima na kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa kwa wananchi wa maeneo hayo.
Ahadi hiyo ilitolewa wakati wa shughuli ya uzinduzi wa Shule ya Awali na Msingi katika Kijiji cha Lesiot, Kata ya Lengatei, ambapo viongozi hao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha miundombinu ya barabara sambamba na uwekezaji katika sekta ya elimu ili kuchochea maendeleo ya wananchi na kuimarisha uhusiano mwema kati ya jamii za Wilaya za Kiteto na Kilindi.

