Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya ETDCO, Mhandisi Richard Mwanja akizungumzia umuhimu wa  Kongamano la Siku ya Nishati (Energy  day) lililofanyika leo, Julai 10, 2026, katika Ukumbi wa Mwandoro, Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano Kampuni ya ETDCO Bi. Samia Chande (kulia) akiwa na Afisa Sheri wa kampuni hiyo Bi. Beatrice Peter  wakifatilia majadiliano katika Kongamano la Siku ya Nishati (Energy  day) lililofanyika leo, Julai 10, 2026, katika Ukumbi wa Mwandoro, Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba)

………….

Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya ETDCO, Mhandisi Richard Mwanja, ameungana na wadau mbalimbali kushiriki Kongamano la Siku ya Nishati (Energy Day) lililofanyika leo, Julai 10, 2026, katika Ukumbi wa Mwandoro, Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mhandisi Mwanja, amesema kuwa ETDCO imejipanga kuendelea kujenga na kukarabati miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme kwa kuzingatia viwango bora vya kitaalamu, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme ya uhakika.

Aidha, amesema ETDCO kama wakandarasi tutahakikisha miradi yote ya ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme inatekelezwa kwa ubora unaokidhi viwango vinavyohitajika, hatua ambayo itachangia upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini.

Mhandisi Mwanja ameeleza kuwa Serikali, kupitia taasisi zake za Sekta ya Nishati, inaendelea kutekeleza mipango na mikakati mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya umeme na kuongeza uzalishaji wa Nishati, kwa lengo la kufikia malengo yaliyowekwa na kuharakisha maendeleo ya Taifa.

Pia amesisitiza kuwa Nishati ya Umeme ina mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi, ikiwemo kuboresha maisha ya wananchi majumbani, kuendesha shughuli za usafirishaji, kukuza viwanda na kuongeza thamani katika uzalishaji na uchakataji wa mazao ya kilimo.

Kongamano hilo limewakutanisha wadau wa Sekta ya Nishati kwa ajili ya kujadili fursa, ubunifu na maendeleo ya sekta hiyo nchini.