Sikuwahi kufikiria kuwa siku moja ningeondoka hospitali nikibeba mzigo wa hofu badala ya furaha. Ilikuwa miezi sita tangu nipate ujauzito wangu wa pili. Kama mama, kila hatua ya ujauzito ilikuwa ya kipekee na ya matumaini.
Nilihudhuria kliniki kama kawaida, nikinywa dawa nilizoelekezwa, na nilikuwa na hamu kubwa ya kumwona mtoto wangu kupitia skani ya pili ya ultrasound. Lakini siku hiyo ilibadilisha kila kitu.
Daktari alikaa kimya kwa muda mrefu kuliko kawaida akitazama skrini. Halafu akahema na kusema kwa sauti ya huruma, “Tunashuku kuna matatizo ya kimaumbile kwenye ukuaji wa kichwa cha mtoto.” Kwa muda ule, nilihisi ulimwengu umesimama.
Alieleza kuwa vipimo vinaonyesha mtoto anaweza kuwa na matatizo ya kiafya ya kudumu na huenda asiwe na uwezo wa kuona wala kusikia. Nilihisi miguu ikikosa nguvu. Nilipotoka hospitali, machozi hayakukoma. Mume wangu alikuwa karibu nami, lakini hata maneno yake hayakunituliza…… SOMA ZAIDI
