Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akiwasilikiliza watumishi wa Mamlaka ya Rufani alipotembelea banda la PPAA kwenye kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).
Na Mwandishi Wetu, Dar
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) ameonesha kuridhika na usimamizi wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) katika matumizi ya Moduli ya kupokea na kushughulukia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST.
Balozi Omar ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la Maonesho la PPAA lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Fedha tarehe 02 Julai 2026 kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo PPAA inaendelea kutoa elimu kwa Umma kuhusu huduma na majukumu yake.
“Hongereni kwa kazi nzuri ya kutoa elimu kwa Umma, nimejulishwa kuwa Kwa sasa baada ya matumizi ya Moduli kuanza hakuna longolongo kwenye mashauri yatokanayo na michakato ya ununuzi wa umma, endeleeni kusimia vyema matumizi ya Moduli vyema,” amesema Balozi Omar
Kwa Upande wake Mkuu wa Sehemu ya Huduma za Sheria PPAA, Bi. Agnes Sayi ambaye alikuwa anamwakilisha Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando alimweleza Mhe. Waziri kuwa kwa mwaka wa fedha 2025/26 Mamlaka ya Rufani imepokea malalamiko takribani 158 yaliyowasilishwa kupitia Moduli hiyo na kuyashughulika kwa wakati kama Sheria ya Ununuzi wa Umma inavyoelekeza.
“Mhe. Waziri matumizi ya moduli yanasaidia Taasisi za Serikali na wazabuni/wadau wa ununuzi kwa ujumla kuokoa muda, gharama, inaongeza uwazi na uwajibikaji, inawezesha utunzaji wa kumbukumbu na kuiwezesha PPAA kutoa hukumu kwa haki na wakati,” amesema Bi. Sayi
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Balozi Hamis ameielekeza PPAA kuendelea kutoa elimu zaidi kwa Umma kuhusu majukumu yake pamoja na matumizi ya Moduli ili kutoa fursa zaidi kwa wazabuni na wadau wa ununuzi wa umma kuendelea kudai haki zao pale ambapo hawakuridhishwa na michakato ya ununuzi wa umma.
Kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 Mamlaka ya Rufani imefanikiwa kutoa elimu kwa wazabuni 1,907 pamoja na watumishi 705 wa idara za ununuzi na sheria katika maeneo mbalimbali nchini katika kanda za Kaskazini, Ziwa, Nyanda za Juu Kusini, Kati, na Pwani pamoja na mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Dodoma, Dar es Salaam, Mbeya, Njombe, Iringa na Mwanza.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mamlaka ya Rufani wakati alipotembelea banda la PPAA kwenye kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha – Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Akomeligwe Kajela Joshua akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Rufani alipotembelea banda la PPAA kwenye kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).

Mmoja kati ya wadau wa Ununuzi wa Umma Bw. Clement Tesha akipokea vipeperushi vinavyoelezea huduma za PPAA wakati alipotembelea banda la PPAA kwenye kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).
Mshiriki wa Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) akijadiliana jambo na watumishi wa PPAA alipotembelea banda la Mamlaka ya Rufani kwenye maonesho hayo.
