Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Ellen Maduhu, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Serbia nchini, Mhe. Jovica Topalović, 1 Julai 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kilimo, baina ya nchi hizo mbili huku yakielezea maendeleo makubwa ya Serbia katika kilimo kama mfano hai wa manufaa ya baadae ya Ushirikiano.

Serbia, ambayo inatambulika Kama miongoni mwa wazalishaji wa mazao ya kilimo barani Ulaya, ilishiriki uzoefu wake katika kilimo cha kisasa na mbinu za kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao.