Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu akizungumza katika hafla ya kupokea gawio na michango kutoka mashirika na taasisi za umma iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam Juni 30, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu wakati akizungumza. 

……………

Msajili wa  Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ameishukuru Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na taasisi mbalimbali za umma kwa ushirikiano na mchango wanaoutoa katika kuiwezesha Serikali kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Akizungumza katika hafla ya kupokea gawio na michango kutoka mashirika na taasisi za umma iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam Juni 30, 2026, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Bw. Mchechu amesema msaada unaotolewa na taasisi kuu za Serikali ikiwemo Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Wizara mbalimbali umechangia kuimarisha utendaji kazi.

“Naomba nishukuru sana kwa msaada tunaoupata kutoka taasisi kuu kama CAG, Ofisi ya AG na Wizara mbalimbali kwani umetuwezesha kwenda kufanya kazi vizuri zaidi,” alisema Mchechu.

Ameeleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha taasisi za umma zinaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia weledi, uwajibikaji na misingi ya utawala bora.