Na Victor Masangu,Pwani 
ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Sophia Simba ameitaka jamii kuwawezesha kiuchumi vijana wa kiume ambao wamesahaulika.
Simba ameyasema hayo Mjini Kibaha wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya Kikundi cha Super Women 2017 na kuwa baada ya wanawake kufanikiwa vijana wakiume nao waangaliwe.
Amesema kuwa kwa muda mrefu jamii iliwekeza kudai haki za wanawake ambapo kwa sasa wamepiga hatua ya kimaendekeo baada ya nguvu kubwa kutumika huku wale wa kiume wakiwa wamesahaulika.
Naye mwanzilishi wa kikundi hicho Betty  Msimbe amesema kuwa wamepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kukopeshana fedha kwa riba nafuu kupitia mfuko wa kikundi kwa fedha wanazoweka ambapo mkopo ni mara tatu ya fedha waliojiwekea.
Kwa upande wake mwenyekiti kikundi hicho Betha Kimambo amesema kuwa wanatarajia kuanzisha mradi wa kukodisha vyombo ili kuongeza kipato ndani ya kikundi.
Naye mratibu wa kikundi hicho Maria Msimbe amesema kuwa wanahamasisha wanawake kujiunga ili kujikomboa kiuchumi.