Na. Fullshangwe Blog, Updates Michezo

Nahodha wa Argentina, Lionel Messi, ameendelea kuongoza orodha ya wafungaji bora katika Kombe la Dunia 2026 baada ya kufikisha mabao sita kufuatia kukamilika kwa hatua ya makundi.

Messi anashika nafasi ya kwanza katika mbio za kuwania tuzo ya Kiatu cha Dhahabu (Golden Boot), huku akifuatiwa na Kylian Mbappé wa Ufaransa, Vinícius Júnior wa Brazil na Erling Haaland wa Norway, ambao kila mmoja amefunga mabao manne.

Kwa upande wa wanaofuatia, Harry Kane wa England, Jonathan David wa Canada na Deniz Undav wa Ujerumani wamefikisha mabao matatu kila mmoja, na kufanya ushindani wa ufungaji kuwa mkali kuelekea hatua ya mtoano.

Michuano ya Kombe la Dunia sasa inaingia hatua ya 32 bora.

ORODHA YA WAFUNGAJI BORA

1. Lionel Messi (Argentina) – 6

2. Kylian Mbappé (France) – 4

3. Ousmane Dembélé (France) – 4

4. Vinícius Júnior (Brazil) – 4

5. Erling Haaland (Norway) – 4

6. Deniz Undav (Germany) – 3

7. Jonathan David (Canada) – 3

8.Ismaila Sarr (Senegal) – 3