Na: Charles Kuzenza
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Naibu Kamishna (DCF) Puyo Nzalayaimisi ametembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa lengo la kujionea shughuli zinazofanywa na Wizara hiyo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea Jijini Dodoma Juni 19, 2026
DCF Nzalayaimisi ameishukuru Wizara hiyo kwa kuendelea kuliunganisha Jeshi hilo na Mahusiano mbalimbali ya Kimataifa na Mashirika ya Nje ambapo Maafisa na Askari wameweza kufaidika na mafunzo mbalimbali

