Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Thobias Andengenye amefanya ziara ya kikazi mkoani Shinyanga kwa lengo la kukagua utendaji kazi wa jeshi hilo na kutoa maelekezo mbalimbali kwa watendaji wa jeshi.
Andengenye amefanya ziara hiyo ya kawaida mkoani Shinyanga kuanzia Juni 16,2019 hadi Juni 17,2019 ambapo pia amekutana na askari ili kujua baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao ya kila siku.
“Nimekuja kufanya ukaguzi wa shughuli za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kujua changamoto kwa kujionea mimi mwenyewe kutoa maelekezo mbalimbali ya makao makuu ya jeshi kwa watendaji waliopo mikoani pamoja na kukutana na kuzungumza na wadau wetu,maafisa na askari”,amesema Andengenye.
Aidha amesema jeshi hilo linaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kukabiliana na majanga huku akiwasisitiza wananchi kuweka kwenye nyumba zao vifaa vya kung’amua na kuzima moto.
Hata hivyo alibainisha kuwa bado kuna changamoto ya vitendea kazi,upungufu wa watumishi na miundombinu isiyo rafiki inayosababisha washindwe kuyafikia baadhi ya maeneo pale matukio yanapotokea
“Ili kukabiliana na changamoto ya vitendea kazi serikali inaendelea kuchukua hatua kwa kutenga bajeti ili kununua vitendea kazi ikiwemo magari na vifaa vingine vya uokoaji”,aliongeza.
Kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akimpokea Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye leo Jumatatu Juni 17,2019. Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga,Omary Simba. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akimzungumza baada ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji nchini, Thobias Andengenye kuwasili ofisini kwake.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye akielezea lengo la ziara yake mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akielezea changamoto zinazolikabili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga kuwa ni pamoja na uhaba wa magari na nyumba za askari wa jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye (kulia),akiagana na Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga wakijiandaa kumpokea Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye katika makao makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye akiwasili katika makao makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye akizungumza na Waandishi wa habari na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye akizungumza na Waandishi wa habari na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga.
Waandishi wa habari na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye akizungumza na Waandishi wa habari na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog