WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Bw. Amin Mawji, Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Shirika la Maendeleo la Aga Khan (AKDN), ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa maendeleo.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, leo Jumatano, Juni 10, 2026.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)