Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 10 Juni 2026, Ikulu Zanzibar, amempokea mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Tharman Shanmugaratnam, na kufanya naye mazungumzo Ikulu Zanzibar pamoja na ujumbe wake.
Rais Tharman aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu nchini Tanzania inayolenga kuimarisha uhusiano wa kirafiki na ushirikiano wa kimaendeleo baina ya Tanzania, ikiwemo Zanzibar, na Jamhuri ya Singapore.

