Na Beda Msimbe, TBN, aliyekuwa Urusi
Kwa miaka mingi, mazungumzo kuhusu nishati nchini Tanzania yamekuwa yakitawaliwa na vyanzo vya maji, gesi asilia, na sasa nishati jadidifu kama jua na upepo.
Hata hivyo, kauli ya hivi karibuni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, , akiwa nchini , imethibitisha kuwa Tanzania sasa imedhamiria kuingia kwenye klabu ya mataifa yanayotumia nishati ya nyuklia ifikapo mwaka 2029.
Hili si jambo la kubahatisha, bali ni mkakati unaoendeshwa na uwepo wa akiba kubwa ya madini ya urani katika Bonde la Mto Mkuju mkoani , mradi unaosubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na fursa zake za maendeleo. Mkakati huu unalenga kuipa nchi vyanzo mbadala na imara vya nishati ili kukabiliana na changamoto za kukatika kwa umeme na ukuaji wa kasi wa sekta ya viwanda.
Historia ya mradi wa urani wa Mkuju River, uliopo ndani ya mfumo wa ikolojia wa Selous na kusini mwa Tanzania, inaonyesha kuwa eneo hilo linatajwa kuwa miongoni mwa hifadhi kubwa zaidi za urani ambazo hazijachimbwa duniani.
Mradi huu unamilikiwa na , ambayo ni kampuni tanzu ya inayomilikiwa na , Shirika la Nishati la Atomiki la Urusi.
Ugunduzi wa madini haya ulileta matumaini makubwa tangu miaka ya 2010 ambapo tafiti za kijiolojia zilionyesha kuwa eneo hilo lina hifadhi inayokadiriwa kufikia tani milioni 152 za miamba yenye madini hayo, inayoweza kuzalisha mamilioni ya ratili za urani iliyosafishwa kwa kiasi fulani kwa zaidi ya miaka 12 hadi 20 ya uhai wa mgodi huo.
Hata hivyo, mradi huo ulikabiliwa na changamoto mbalimbali zilizosababisha usitishwaji wa muda, ikiwemo kuanguka kwa bei ya urani duniani baada ya ajali ya nyuklia ya nchini mwaka 2011.
Mahitaji ya urani duniani yalishuka sana na kupelekea bei kuporomoka, hali iliyoufanya uchimbaji wa Mkuju kutokuwa na tija ya kibiashara kwa wakati huo.
Changamoto nyingine ilikuwa ni mazingira na udhibiti, kwa kuwa eneo la mradi lilikuwa ndani ya Hifadhi ya Selous ambayo ni eneo la Urithi wa Dunia, jambo lililoilazimisha serikali kufanya mabadiliko ya mipaka ili kuruhusu uchimbaji bila kuathiri ikolojia nzima ya eneo hilo.
Baada ya usingizi wa muda mrefu, mradi wa Mkuju sasa unafufuka kwa kasi kubwa kutokana na kupanda upya kwa bei ya urani duniani pamoja na msukumo wa kisiasa kutoka kwa serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa sasa, na wamekamilisha hatua za majaribio ya teknolojia ya uchenjuaji iitwayo In-Situ Recovery pamoja na majaribio ya kinu cha majaribio.
Teknolojia hii ni ya kisasa na salama zaidi kimazingira kwani haihusishi uchimbaji wa mashimo makubwa, bali huingiza vimiminika maalum ardhini vinavyoyeyusha urani na kuivuta juu ikiwa katika mfumo wa kimiminika.
Mazingira ya sasa yanaonyesha kuwa miundombinu ya msingi ikiwemo barabara za kuingia eneo la mradi, mifumo ya ulinzi wa mionzi, na kambi za wafanyakazi tayari imeimarishwa huku serikali kupitia ikiendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha usalama wa mionzi unazingatiwa kabla ya uchimbaji kuanza kikamilifu.
Ukimya wa miaka kadhaa uliacha maswali mengi, lakini sasa wananchi na wadau wa kiuchumi wanasubiri kwa shauku kubwa kuanza kwa mgodi huu kutokana na fursa za ajira na ukuaji wa uchumi wa ndani.
Wakazi wa mikoa ya Kusini hasa na wanatarajia kupata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja pamoja na kukuza biashara za ndani kupitia usambazaji wa bidhaa mgodini.
Mradi huu pia unatajwa kuwa chanzo kipya na kikubwa cha mrabaha na kodi kwa serikali, fedha ambazo zinaweza kusaidia kufadhili miradi mingine ya kijamii kama afya na elimu.
Aidha, matumaini ya uhuru wa nishati yanaendelea kuongezeka baada ya kauli ya Rais Samia kuwa urani hiyo itatumika kuzalisha umeme nchini. Kauli hiyo inaleta matumaini mapya kuwa Tanzania haitakuwa tu msafirishaji wa malighafi, bali pia mtumiaji wa mwisho wa teknolojia hiyo.
Uthibitisho mkubwa zaidi unaoonyesha kuwa Tanzania inaelekea kuwa na kinu cha nyuklia kwa umakini mkubwa ni uwepo wa mkataba wa faragha unaozuia pande mbili, yaani na , kutoa taarifa wakati mazungumzo yakiendelea hadi yatakapofikia hatua ya mwisho.
Wataalamu wa sekta ya nishati na sheria nchini wameeleza kuwa mikataba ya aina hiyo ni ya kawaida lakini huwa ya kiwango cha juu sana inapohusisha masuala nyeti ya usalama na nishati ya kimkakati kama nyuklia.
Usiri huo unalenga kulinda maslahi ya taifa na kuzuia kuingiliwa kwa mazungumzo hayo na mataifa mengine au washindani wa kijiografia kabla ya makubaliano kukamilika rasmi.
Hatua hiyo ya usiri inatafsiriwa na wachambuzi kama ishara ya wazi kuwa pande zote mbili ziko katika hatua za mwisho za kiufundi na kisheria kufanikisha ujenzi wa kinu hicho bila kuleta taharuki.
Ili kufikia maono ya mwaka 2029 ya kuwa na kinu cha nyuklia, Tanzania inakabiliwa na jukumu kubwa la kujenga mfumo madhubuti wa udhibiti wa kisheria na kitaalamu.
Rais Samia, akizungumza na waandishi wa habari mjini wakati akihudhuria , alibainisha kuwa sasa itakuwa na kazi kubwa inayohusiana na matumizi ya nyuklia kwa amani kwa kuzingatia maelekezo ya .
Ushirikiano mpya na Urusi hautalenga tu kununua mitambo, bali pia kuhamisha teknolojia kwa kutoa mafunzo kwa wahandisi wa Kitanzania wanaofadhiliwa masomo nchini Urusi.
Hili ni jambo muhimu sana kwa sababu usalama wa kinu cha nyuklia unategemea kwa kiwango kikubwa uwezo, maarifa, na umakini wa wataalamu wanaokisimamia.
Wataalamu wa nishati kutoka serikalini wanasisitiza kuwa hatua hii ya kimkakati itaiwezesha Tanzania kuwa na uhakika wa nishati ya viwanda ambayo haitayumba kutokana na mabadiliko ya tabianchi kama ilivyo kwa nishati ya maji.
Kauli hizo ziliungwa mkono na Rais Samia Suluhu Hassan aliyesema kuwa lengo la serikali ni kufikia uzalishaji wa megawati 8,000 za umeme ili kuwa na ziada ya kuuza katika nchi jirani.
Mazungumzo yanayoendelea chini ya mkataba wa faragha yanalenga kuhakikisha kuwa ujenzi wa kinu hicho unazingatia viwango vyote vya kimataifa pamoja na gharama zinazoweza kubebwa na uchumi wa Tanzania.
Hii inaonyesha kuwa serikali haikurupuki, bali inasonga mbele kwa hatua madhubuti zilizofanyiwa tafiti za kina ili kulinda maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho.
Safari ya kuelekea mwaka 2029 tayari imeanza kwa kasi kubwa na kwa umakini chini ya usimamizi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Ziara yake nchini Urusi, pamoja na mafanikio yake ya kisiasa na kiuchumi, imefungua njia ya mikataba kadhaa inayogusa teknolojia ya nyuklia.
Urani ya Mkuju si hadithi tena ya madini yaliyolala ardhini, bali ni mtaji wa kimkakati unaoweza kubadilisha kabisa ramani ya nishati katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati.
Iwapo ahadi ya Rais Samia itatimia na mazungumzo ya sasa yakazaa matunda yaliyokusudiwa, ifikapo mwaka 2029 moshi na mwanga kutoka kwenye kinu cha kwanza cha nyuklia cha Tanzania vitakuwa ushahidi wa taifa lililoamua kuikumbatia nishati ya kesho kwa ajili ya maendeleo endelevu ya leo.
