Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa washiriki wa kozi kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa cha India walipotembelea Ofisi za iliyokuwa Makao Makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Juni 26.
Akizungumza na washiriki wa kozi hiyo, Jenerali Mkunda amesisitiza kuendelea kwa ushirikiano wa kimafunzo kati ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la India ili kuwajengea uwezo kijeshi wanajeshi wa nchi mbili hizi.
“Tunashuru kwa kuja kuitembelea Tanzania kwa ziara ya kimafunzo, hii inaonesha jinsi diplomasia ya kijeshi inavyochangia kuongeza weledi na ujuzi kijeshi.
Naye, Mkuu wa msafara wa washiriki wa kozi hiyo Rear Admiral…amesema kuwa, kundi la washiriki wa kozi ya NDC India wamejionea jinsi JWTZ linavyoboresha mafunzo yake, na kupongeza maendeleo ya kimafunzo kwa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (Command and Staff Collage) kilichopo Duluti Jijini Arusha.
Aidha, Rear Admiral…alipongeza juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza sekta ya utalii nchini na kuvutiwa na mazingira ya Bonde la Ngorongoro lenye wanyama pori ndani yake.
Ujumbe wa Washiriki wa Kozi kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha nchini India uliowasili nchini tarehe 31 Machi 26 unatarajia kukamilisha ziara ya kimafunzo nchini, na kurejea nchini India leo.


