Na Victor Masangu, Kibaha

Jumuiya ya Umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha katika kuimarisha kasi ya Uhai  wa jumuiya yao pamoja na kuongeza idadi ya wanachama imeamua kukutana  na  makatibu wa uwt ngazi zote za kata kwa lengo la kuweza kujadili mambo mbali mbali ambayo yataweza kuleta tija  na ufanisi zaidi katika utekelezaji wa majukumu katika maeneo  wanayotokea kuanzia ngazi za chini.

Katika kikao kazi hicho ambacho kimeandaliwa na katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha Cecilia Ndaru pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Elina Mgonja kitaweza  kuwakutanisha makatibu hao ngazi ya  Kata  kwa lengo la kuweza kujadili mambo mbali mbali yanayohusu jumjuiya hiyo sambamba na kuangalia jinsi ya kuimarisha jumuiya hiyo pamoja na kukumbushana mambo mbali mbali.

Katibu  Ndaru amesema kwamba kwa sasa lengo  lao kubwa ni la kuwakutanisha makatibu hao ni  pamoja na kuweka mipango madhubuti ambayo itasaidia  katika kuongeza kasi ya wanachma katika jumuiya hiyo ikiwa sambamba na kukumbushana umuhimu wa kufanya vikao  vya kikatiba ambavyo ndio nguzo imara katika kuijenga jumuiya yao.

Pia amegusia suala la kuwa na mshikamano wa pamoja  na kuweza kushirikiana bega kwa bega na wanawake wenzao lengo ikiwa ni  kuweka misingi imara ambayo iataweza kusaidia katika kuboresha utendaji wa kazi katika maeneo yao.

“Leo tumekutana na makatibu wa umoja wa wanawake wa UWT katika ngazi za kata mbali mbali na tumeweza kujadili mambo mbali mbali  ikiwemo suala la kuweka mikakaati na kukumbushana jinsi ya uhai wa jumuiya yetu pamoja na mambo mengine mbali mbali ya maendeleo,”amebainisha Katibu Ndaru

Katika hatuua nyingine Katibu huyo amewahimiza makatibu hao ngazi ya  kata kuhakikisha kwamba wanakuwa wanashirikiana na wanawake wenzao katika  suala zima la kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika nyanja mbali mbali.

Nao baadhi ya makatibu wa uwt ngazi ya kata ambao wamehudhulia kikao kai hicho wamesema kwamba  watakwenda kuyafanyia kazi yale yote ambayo wameelekezwa na Katibu pamoja na Mwenyekiti wao na kwamba lengo  ni kuendelea kushikamana kwa pamoja kwa maslahi ya jumuiya yao pamoja na chama.

Katika kikao kazi hicho kimejadili ajenda mbali mbali ikiwemo suala zima la  umuhimu wa ushiriki wa vikao, kupeana taarifa za utendaji, kusoma taarifa ya mapato na matumizi, kuweka mikakati ya kuingiza wanachama wapya  ambao wataweza kusaidia katika  kuimarisha uhai wa jumuiya pamoja na chama.