Na Victor Masangu, Kibaha
Jumuiya ya Umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha katika kuimarisha kasi ya Uhai wa jumuiya yao pamoja na kuongeza idadi ya wanachama imeamua kukutana na makatibu wa uwt ngazi zote za kata kwa lengo la kuweza kujadili mambo mbali mbali ambayo yataweza kuleta tija na ufanisi zaidi katika utekelezaji wa majukumu katika maeneo wanayotokea kuanzia ngazi za chini.
Katika kikao kazi hicho ambacho kimeandaliwa na katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha Cecilia Ndaru pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Elina Mgonja kitaweza kuwakutanisha makatibu hao ngazi ya Kata kwa lengo la kuweza kujadili mambo mbali mbali yanayohusu jumjuiya hiyo sambamba na kuangalia jinsi ya kuimarisha jumuiya hiyo pamoja na kukumbushana mambo mbali mbali.
Katibu Ndaru amesema kwamba kwa sasa lengo lao kubwa ni la kuwakutanisha makatibu hao ni pamoja na kuweka mipango madhubuti ambayo itasaidia katika kuongeza kasi ya wanachma katika jumuiya hiyo ikiwa sambamba na kukumbushana umuhimu wa kufanya vikao vya kikatiba ambavyo ndio nguzo imara katika kuijenga jumuiya yao.
Pia amegusia suala la kuwa na mshikamano wa pamoja na kuweza kushirikiana bega kwa bega na wanawake wenzao lengo ikiwa ni kuweka misingi imara ambayo iataweza kusaidia katika kuboresha utendaji wa kazi katika maeneo yao.
“Leo tumekutana na makatibu wa umoja wa wanawake wa UWT katika ngazi za kata mbali mbali na tumeweza kujadili mambo mbali mbali ikiwemo suala la kuweka mikakaati na kukumbushana jinsi ya uhai wa jumuiya yetu pamoja na mambo mengine mbali mbali ya maendeleo,”amebainisha Katibu Ndaru
Katika hatuua nyingine Katibu huyo amewahimiza makatibu hao ngazi ya kata kuhakikisha kwamba wanakuwa wanashirikiana na wanawake wenzao katika suala zima la kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika nyanja mbali mbali.
Nao baadhi ya makatibu wa uwt ngazi ya kata ambao wamehudhulia kikao kai hicho wamesema kwamba watakwenda kuyafanyia kazi yale yote ambayo wameelekezwa na Katibu pamoja na Mwenyekiti wao na kwamba lengo ni kuendelea kushikamana kwa pamoja kwa maslahi ya jumuiya yao pamoja na chama.
Katika kikao kazi hicho kimejadili ajenda mbali mbali ikiwemo suala zima la umuhimu wa ushiriki wa vikao, kupeana taarifa za utendaji, kusoma taarifa ya mapato na matumizi, kuweka mikakati ya kuingiza wanachama wapya ambao wataweza kusaidia katika kuimarisha uhai wa jumuiya pamoja na chama.

