Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (anayeshughulikia huduma za Hazina), Bw. Nsubili Joshua, akizungumza jambo wakati akifunga Mkutano wa 39 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha kwa mwaka 2025/26 uliofanyika katika Ukumbi wa Kambarage (Treasury Square) jijini Dodoma.

Kaimu Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Fedha Bw. Shumbi Jackson, akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Mkutano wa 39 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha kwa mwaka 2025/26 uliofanyika katika Ukumbi wa Kambarage (Treasury Square) jijini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Fedha, wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (anayeshughulikia huduma za Hazina), Bw. Nsubili Joshua, wakati akifunga rasmi Mkutano wa 39 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha kwa mwaka 2025/26 uliofanyika katika Ukumbi wa Kambarage (Treasury Square) jijini Dodoma.

Meza Kuu ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (anayeshughulikia huduma za Hazina), Bw. Nsubili Joshua (Katikati), wakisikiliza hoja mbalimbali za wajumbe wakati wa Mkutano wa 39 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha kwa mwaka 2025/26 uliofanyika katika Ukumbi wa Kambarage (Treasury Square) jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Kaimu Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Fedha Bw. Shumbi Jackson (kulia) na Mjumbe wa Mkutano huo ambaye pia ni Kaimu Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mhandisi Kenneth Nindie (kushoto)

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Fedha, Bw. Simbani Liganga, (kushoto), akisalimiama na Kaimu Kamishna, Kitengo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, katika Ukumbi wa Mikutano Kambarage, wakati wa Mkutano wa 39 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha kwa mwaka 2025/26 uliofanyika katika Ukumbi wa Kambarage (Treasury Square) jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (anayeshughulikia huduma za Hazina), Bw. Nsubili Joshua (kushoto), akiagana na Kaimu Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Fedha Bw. Shumbi Jackson, baada ya kufunga Mkutano wa 39 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha kwa mwaka 2025/26 kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El maamry Mwamba, uliofanyika katika Ukumbi wa Kambarage (Treasury Square) jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha – Dodoma)

…………

Na. Peter Haule na Jordan Mbwambo, WF, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Nsubili Joshua amewataka watumishi wa Wizara hiyo kudumisha mshikamano, nidhamu, weledi na uzalendo katika kutekeleza majukumu ya kila siku ili kuwezesha kufikia malengo ya Wizara na Taifa kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha 39 cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha kilichofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 28 hadi 29 Mei 2026.

Alisema kuwa wajumbe wa Baraza hilo wanatakiwa kuwa mabalozi wazuri katika kuhakikisha maazimio na mapendekezo yote yaliyotokana na mijadala iliyokuwepo inazingatiwa kikamilifu na kufanyiwa kazi kwa wakati ili kuendelea kuimarisha ufanisi, uwajibikaji na mazingira bora ya kazi kwa watumishi wote wa Wizara.

Aidha, amewapongeza wajumbe wa Baraza hilo kwa mijadala yenye tija, maoni ya kujenga na michango yenye hekima, busara na mtizamo wa kuboresha utendaji wa wizara.

Alisema mada zote zilizowasilishwa zimegusa maeneo muhimu yanayohusu utendaji wa Wizara, ustawi wa watumishi pamoja na utekelezaji wa majukumu ya msingi ya kusimamia uchumi na fedha za umma.

Kwa upande mwingine Afisa Habari wa Wizara hiyo, Bw. Joseph Mahumi, amewataka wajumbe wa Baraza kutumia akaunti rasmi za mitandao ya kijamii ya Wizara ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu mafanikio na mikakati mbalimbali ya Wizara, Sera na masuala ya uchumi na fedha.

“Kwa upande wa Akaunti ya LinkedIn Wizara imefanya vizuri si tu kwa Wizara na Taasisi za Serikali lakini pia kwa taasizi binafsi zikiwemo Benki na mashirika binafsi, jambo ambalo si la kubeza”, alisema Bw. Mahumi.

Amesema pia Wizara inafanya vizuri katika mitandao ya Instagram (urtmof), Facebook (MofURT), Youtube (Hazina TV), LinkedIn (Ministry of Finance Tanzania), Whatsapp Channel (Wizara ya Fedha Tanzania) na Threads (urtMof).

Amewataka watanzania kwa ujumla kufuatilia kwa karibu mitandao hiyo ili kupata taarifa muhimu za masuala ya Sera, fedha na programu mbalimbali zitakazowasaidia kufanya maamuzi sahihi katika kukuza maendeleo binafsi na ya Taifa kwa Ujumla.