Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili katika Viwanja vya Kilimani Wilayani Chato Mkoani Geita, ambapo anaungana na waombolezaji mbalimbali kushiriki Ibada ya kumuaga na kumuombea Marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli ambaye ni Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, inayofanyika leo tarehe 29 Mei 2026.