Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Vijana ya Tanzania, Serengeti Boys, imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 (AFCON U-17) baada ya kuiondoa Misri katika mchezo wa nusu fainali kwa mikwaju ya penalti, kufuatia mchezo huo kumalizika kwa sare tasa.

Serengeti Boys ilifanikiwa kushinda kwa penalti 4-3 katika mchezo huo wa nusu fainali.

Kutokana na matokeo hayo, Serengeti Boys katika mchezo wa fainali watacheza dhidi ya Senegal, ambayo iliiondoa Morocco katika mchezo mwingine wa nusu fainali.