Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Dodoma
serikali imewaelekeza wakurugenzi wa halmashauri pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali za umma nchini kuacha mara moja tabia ya kuzuia au kuchelewesha barua za uhamisho kwa watumishi wa umma, ikieleza kuwa hatua hiyo ni kinyume na taratibu za kiutumishi na inaweza kuathiri haki pamoja na ufanisi wa watumishi katika utekelezaji wa majukumu yao.,
Maelekezo hayo yametolewa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB), Bw. Juma Mkomi, Mei 26,2026 Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari , Aidha, Mkomi amesema kikao hicho kitawakutanisha viongozi kutoka Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mkomi amesema hakuna kiongozi mwenye mamlaka ya kuwazuia watumishi wa umma kuhamia katika vituo vingine vya kazi iwapo taratibu zote za kiutumishi zimezingatiwa, akisisitiza kuwa viongozi wanapaswa kushughulikia maombi ya uhamisho kwa wakati na kwa kuzingatia sheria pamoja na kanuni zilizopo.
amefafanua kuwa ucheleweshaji wa barua za uhamisho unaweza kuathiri utendaji kazi wa watumishi pamoja na maisha yao ya kila siku, hivyo viongozi wanatakiwa kuondoa vikwazo visivyo vya lazima vinavyoweza kudhoofisha mazingira ya kazi serikalini.
kwa upande mwingine, Mkomi amesema tathmini iliyofanywa mwezi machi mwaka huu imebaini kuwa kukamilika kwa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kumeongeza mahitaji ya watumishi katika sekta tofauti za umma.
amesema hadi sasa serikali inakabiliwa na upungufu wa takribani watumishi laki mbili, hali inayohitaji mikakati madhubuti ya kuongeza nguvu kazi ili kuendana na kasi ya utoaji wa huduma kwa wananchi.
