Afisa Mradi kutoka Shirika la Blue Cross Society of Tanzania, Glory Vincent Pagundile, akizungumza katika semina hiyo na waandishi wa habari

………….
Na Happy Lazaro, Arusha
VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kutumia kalamu zao vizuri kwani vina nafasi kubwa katika kupunguza madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya, pombe na tumbaku kwa kutoa elimu hiyo kwa jamii.
Hayo yamesemwa na Afisa Mradi kutoka Shirika la Blue Cross Society of Tanzania, Glory Vincent Pagundile, wakati akizungumza katika semina na waandishi wa habari iliyoandaliwa na shirika hilo chini ya mpango wa Afya kwa vijana na jamii, Zuia Madhara yajayitokana na dawa za kulevya na pombe, iliyolenga kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika kampeni za utoaji elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya pamoja na changamoto zinazoendelea kuikabili jamii ikiwemo ukatili unaotokana na matumizi ya dawa za kulevya.
Amesema kuwa,bado ipo haja kubwa ya kuongeza elimu kwa wananchi kwani vijana wengi wanaendelea kuathirika kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi kuhusu madhara ya matumizi ya dawa.
“Hivyo tunaziomba mamlaka husika kuendelea kusimamia kwa karibu mapambano dhidi ya dawa za kulevya, pombe na tumbaku ili kuokoa nguvu kazi ya taifa hasa vijana,” aamesema.
Glory amesema pamoja na changamoto hizo, shirika hilo limeanza kuona matokeo chanya kupitia kampeni zake za elimu ambapo baadhi ya vijana waliokuwa katika hatari ya kuanza matumizi ya dawa za kulevya wamebadili mitazamo yao baada ya kupata elimu.
Alisema pia baadhi ya waliokuwa tayari wameathirika wameonyesha mabadiliko na kuamua kuacha matumizi ya dawa hizo baada ya kupata elimu na ushauri.
Katika hatua nyingine, alisema shirika hilo limefanikiwa kuwafikia zaidi ya watu 20,000 kupitia kampeni mbalimbali za elimu, mafunzo kwa viongozi wa kata na mitaa pamoja na vijana wanaopewa elimu rika ili nao wawe mabalozi wa kuelimisha wenzao.
Kwa mujibu wa Glory, shirika hilo linaamini kuwa elimu inayotolewa kupitia redio, televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii ina uwezo mkubwa wa kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa wakati mmoja tofauti na elimu inayotolewa katika maeneo machache ya mikutano au madarasa.
“Tunapoingia kwenye vyombo vya habari tunapata nafasi ya kuwafikia watu wengi zaidi. Ndiyo maana tunaendelea kushirikiana na waandishi wa habari ili kuhakikisha taarifa sahihi zinaifikia jamii kwa wakati,” amesema.
Glory amefafanua kuwa,bado kuna changamoto ya upatikanaji wa takwimu sahihi zinazohusu matumizi ya dawa za kulevya pamoja na uwepo wa mitazamo hasi na baadhi ya tamaduni zinazochangia kuendelea kwa tatizo hilo katika jamii.
Ameongeza kuwa wakati mwingine vitendo vya rushwa na uzembe wa baadhi ya watu vinachangia elimu na taarifa sahihi kutowafikia wananchi ipasavyo.
“Tunaziomba mamlaka husika kuendelea kusimamia kwa karibu mapambano dhidi ya madawa ya kulevya kwani swala hilo ni la kila mmoja wetu kwa pamoja katika kushirikiana .”amesema
Glory amesema pamoja na changamoto hizo, shirika hilo limeanza kuona matokeo chanya kupitia kampeni zake za elimu ambapo baadhi ya vijana waliokuwa katika hatari ya kuanza matumizi ya dawa za kulevya wamebadili mitazamo yao baada ya kupata elimu.
Amesema pia baadhi ya waliokuwa tayari wameathirika wameonyesha mabadiliko na kuamua kuacha matumizi ya dawa hizo baada ya kupata elimu na ushauri.
Katika hatua nyingine, ameongeza kuwa, shirika hilo limefanikiwa kuwafikia zaidi ya watu 20,000 kupitia kampeni mbalimbali za elimu, mafunzo kwa viongozi wa kata na mitaa pamoja na vijana wanaopewa elimu rika ili nao wawe mabalozi wa kuelimisha wenzao.
Amefafanua kuwa, bado ipo haja kubwa ya kuongeza elimu kwa wananchi kwani vijana wengi wanaendelea kuathirika kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi kuhusu madhara ya matumizi ya dawa hizo.
“Waandishi wa habari ni kiungo muhimu sana katika mapambano haya. Kupitia kalamu zao wana uwezo mkubwa wa kuelimisha jamii na kusaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi kuhusu maisha yao,” amesema Glory.
Ameongeza kuwa Blue Cross Society of Tanzania imejikita katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya dawa za kulevya, pombe, tumbaku pamoja na masuala ya ukatili wa kijinsia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari.
“Tunawajengea uwezo vijana ili waweze kutoa elimu kwa vijana wengine. Tunaamini njia hiyo itasaidia ujumbe kufika kwa watu wengi zaidi na kusaidia kupunguza madhara ya dawa za kulevya kwenye jamii,” amesema.
Amesisitiza kuwa Blue Cross Society of Tanzania itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari pamoja na taasisi mbalimbali kuhakikisha jamii inapata elimu sahihi itakayosaidia kujenga taifa lenye vijana wenye maadili na afya bora.
