Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Joseph Mkude akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo kuhusu mgomo wa daladala.
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Joseph Modest Mkude amesema Jiji la Arusha linaendelea kuwa salama na wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida kufuatia taarifa zilizozagaa kuhusu madai ya mgomo wa daladala katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Mkude amesema Serikali ilifanya kikao cha haraka pamoja na wadau wa usafirishaji ikiwemo viongozi wa daladala na mamlaka husika ili kusikiliza changamoto zilizojitokeza na kutafuta suluhisho la pamoja.
Amesema baadhi ya changamoto zilizowasilishwa ni pamoja na malalamiko ya kuingiliwa kwa route za daladala, tozo mbalimbali pamoja na maboresho ya mfumo wa utoaji wa faini kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri.
Aidha, amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote wa sekta ya usafirishaji kuhakikisha huduma zinaendelea kutolewa kwa wananchi kwa usalama, ufanisi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Aidha Mkude amewataka madereva na watoa huduma za usafiri kuendelea kuwahudumia wananchi kwa weledi huku akisisitiza kuwa Arusha ipo tulivu na hakuna sababu ya wananchi kuwa na hofu.
“Hakuna nauli inayozidi kiasi cha 1,000 wanatakiwa kujua hilo ,zaidi ya kilometa nane hatakiwi kutoza elfu moja hadi itakapotangazwa na swala la bei haitakiwi kutozwa kama wanavyotaka wao.
Aidha Mkude amewataka wananchi hao kuwe watulivu wakati serikali inaendelea kushughulikia swala hilo la kupanda kwa nauli mpaka Arusha iwe sawa .
“Kamati ya usalama mkoa inahakikisha wanaendelea kuwalinda wananchi na kuhakilisha wanafanya shughuli zao kama.kawaida bila kuwepo kwa changamoto yoyote.”amesema .
Aidha amefafanua kuwa kutokana na mgomo huo baadhi ya viongozi wa daladala wamekamatwa kutokana na kuwakataza watu wasiendeshe magari yao .
“Bei ya mafuta ipo juu na swala la mafuta ni swala la ulimwengu sio Arusha peke yake hivyo Kwa nini Arusha tuone mafuta ndo yanatuumiza zaidi kuliko wengine wakati.janga hilo nili nchi nzima .”amesema .
“Sisi wote hata mimi hatuna mamlaka ya kupanga bei kuna chombo kina mamlaka hiasika ambacho kina mamlaka ya kupandisha nauli na naombeni mkasimamie bei zilizopangwa na kamwe naombeni sana watu wasiende kinyume na hapo.”amesema Mkude .
Aidha akizungumzia kuhusu swala la kupanga route kulingana na mazingira ya Arusha amesema kuwa route zote zitapangwa na viongozi husika na kamwe wasijipangie route wenyewe wasubiri mamkala husika .
