Mkurugenzi wa Makumbusho ya Kumbukumbu ya  Chifu Ndaskoi  akizungumza kwenye hafla hiyo jijini Arusha leo.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Kumbukumbu ya  Chifu Ndaskoi akitoa maelezo kuhusu makumbusho hiyo kwa naibu meya pamoja na vuongozi mbalimbali waliotembelea makumbusho hayo.
……………
Na Happy Lazaro, Arusha
Kwa mara ya kwanza tangu kuanzisha mwaka 2016, Makumbusho ya Kumbukumbu ya Chifu Ndaskoi imeadhimisha Siku ya Makumbusho Duniani ikiongozwa na Kaulimbiu isemayo; “Miti na utamaduni; kuunganisha zamani na kesho”
Wakati wa sherehe hiyo Wadau mbalimbali pamoja na jamii wamehimizwa kuchukua hatua za makusudi kuenzi, kuhifadhi na kuridhisha utamaduni wetu wa Kiafrika ili kuthibiti mmomonyoko wa maadili unaoikabili ya jamii.
Aidha, wazazi wameombwa kuwajibika ipasavyo katika malezi ya watoto na vijana na vijana kuacha kukumbatia  utandawazi bila kuangalia madhara yake.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Kumbukumbu ya  Chifu Ndaskoi iliyopo kata ya Moshono Jijini Arusha, Ol-aiguenani Meshack  Ndaskoi kwenye hafla  ya kuadhimisho ya siku ya makumbusho duniani, iliyofanyika kwa kupanda miti ya asili zaidi ya  mia  moja katika eneo la Bustani ya kuhifadhi miti ya asili na mazingira ambayo ni sehemu ya Makumbusho hiyo.
Aidha  miti  hiyo ya  asili  ilioteshwa kama njia ya kudumisha utamaduni kwa sababu zinatumika katika masuala ya kiroho,  madawa. rasilimali na chakula, utamaduni. Kuhifadhi na kutunza miti ya asili kuzuia katika hataria ya kupotea  kutokana na shughuli za kibinadamu na mabadiliko ya tabia nchi.
Ameendelea kusema kuwa, jitihada za makusudi zinahitajika za kuweka mikakati madhubuti ya kuhifadhi mila na desturi zetu za Kiafrika kwa kuandaa mzingira yatakayohakikisha kwamba tunaridhisha mila na desturi zetu nzuri kwa vizazi vijavyo.
Kuondokana changamoto za kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili unaochangia ukosefu  wa  nidhamu pamoja na vijana wengi kupotea kimaisha.
‎Ndaskoi amesema kuwa, kutokana na utandawazi hivi sasa jamii nyingi zimeanza kuacha  misingi ya malezi ya kiafrika jambo linalosababisha jamii hususan vijana kukosa uadilifu, heshima,  ujasiri, umoja na mshikamano ndani ya jamii.
Ndaskoi amesema kuwa, makumbusho hiyo inajikita zaidi katika kuonyesha historia ya Arusha tangu mwishoni mwa karne ya 16  na Utamaduni wa jamii ya Wamaasai ambapo inatoa fursa kwa wadau pamoja na watu mbalimbali kujifunza na kujionea mambo mbalimbali kuhusu tulikotoka, tuloko ambayo ni muhimu katika kuleta maendeleo endelevu tunakokwenda.
“Makumbusho hii inatoa fursa pia kwa wanafunzi wa Shule za Maingj na Sekondari na vyuo na hata watalii kuweza kutembelea na kujifunza maswala mbalimbali  ambayo yamesahaulika na yanatakiwa kuenziwa.
Alitoa wito kwa wadau mbalimbali kuwezesha Makumbusho haya  kuendelea kuwaidia jamii kuenzi mila na desturi zetu ili zisisahaulike katika jamii.
Naye Naibu Meya wa Jiji la ArushaJulius Ole Sekeyan  akizungumza kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha  Maxmilian Iranghe amesema kuwa, jambo lililofanywa na Ol-aiguenani Meshack Ndaskoi la kuanzisha Makumbusho haya binafsi ni jambo zuri na linapaswa kuungwa mkono na wdau wote kwa kiwango kikubwa sana .
Amesema kuwa, Serikali ipo tayari kushirikiana  kwa karibu sana na  Makumbusho ya kumbukumbu ya  Chifu Ndaskoi ambayo inalenga kuhifadhi na kukuza historia na desturi na mila za Wamaasai.
“Jitihada hizi zisizopigiwa upatu zilizofanywa na mwenzetu huyu ni kubwa na zinapaswa kuungwa mkono sana kwani zinasaidia sana kutukumbusha na kuenzi mila na desturi za jamii zetu kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na  vijavyo katika kudumisha utamaduni .”amesema .
Diwani wa kata ya Moshono, Ciriliel Mbise amewataka wananchi wa jiji la Arusha kujitokeza kwa wingi kutembelea makumbusho hiyo ili kuweza kujifunza historia ya Arusha na utamdaduni  wa jamii ya Wamaasai na kuweza kuziendeleza.
Aidha Mbise ameitaka jamii kuenzi na kuthamini tamaduni zao ili kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuvamiwa na utandawazi ambao umechangia kuporomoka kwa maadili katika jamii.