Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (kushoto) akiongoza zoezi la Usafi wa Mazingira katika kituo cha daladala na bajaji (Stendi ya Kabwe) kilichopo Kata ya Iyela, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Jijini Mbeya, leo Mei 24, 2026. Zoezi hilo la Usafi wa Mazingira limefanyika ikiwa ni Kampeni Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 2026 ambayo kitaifa yatafanyika Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center, Juni 5, 2026.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais walioambatana naye kutoka Dodoma mara baada ya kushiriki zoezi la Usafi wa Mazingira lililofanyika katika kituo cha daladala na bajaji (Stendi ya Kabwe) kilichopo Kata ya Iyela, jijini Mbeya, leo Mei 24, 2026. Waliokaa chini upande wa kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Lodrick Mpogolo na Diwani wa Kata ya Iyela, Absalom Kubombaki Mwambepo. Upande wa kushoto ni Naibu Meya wa Jiji la Mbeya, Kephas Mwasote na Meneja wa NEMC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Josia Mlunya.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akizungumza na wananchi katika Stendi ya Kabwe iliyopo Kata ya Iyela, jijini Mbeya, mara baada ya kukamilisha zoezi la Usafi wa Mazingira lililofanyika katika stendi hiyo, ikiwa ni sehemu ya Kampeni Maalumu kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 2026.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akipanda mti katika viwanja vya Shule ya Msingi Tembela iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, jijini Mbeya, leo Mei 24, 2026, ikiwa ni sehemu ya Kampeni Maalumu ya Upandaji Miti na Usafi wa Mazingira kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 2026.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Tembela iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Jijini Mbeya, leo Mei 24, 2026 ikiwa ni muda mfupi kabla ya zoezo la Upandaji Miti katika shule hiyo ikiwa ni Kampeni Maalumu Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniania 2026.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt Richard Muyungi (kulia) amekabidhi kiasi cha fedha taslimu kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tembela, Bi. Leah Ijumba Mwaipaja, kwa ajili ya ununuzi wa majagi ya kumwagilia miti shuleni hapo. Zoezi hilo limefanyika leo Mei 24, 2026, Jijini Mbeya, kama sehemu ya Kampeni Maalumu Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 2026, yatakayofanyika kitaifa Juni 5, 2026 Jijini Dodoma.
KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA SHIRIKI KUFANYA USAFI STENDI YA KABWE JIJINI MBEYA
