Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 20 Mei 2026, katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Kikombo Dodoma, amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu 6 wa Mikoa ya mpakani ya Tanzania waliomtembelea kwa ajili ya kujadiliana na kuimarisha masuala ya Ulinzi na Usalama wa nchi.
Wakuu wa Mikoa hiyo waliokutana na Waziri wa Ulinzi na JKT ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe CPA,Amos Makalla, Mhe. Balozi Batilda Burian ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mkuu wa mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Mtambi na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Jabir Makame, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Yahya Kido, pia katika kikao hicho alikuwepo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe, Kanali Donald Msengi.
Aidha, Wakuu hao wa Mikoa ya Mipakani walipata fursa ya kutembelea Ofisi za Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa na kujionea jinsi inavyofanya kazi.

