Na Kassim Nyaki, Dodoma.

Leo tarehe 18 Mei, 2026 waheshimiwa wabunge wataendelea kujadili bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliyowasilishwa ijumaa iliyopita na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Dkt. Ashatu Kijaji ikitaja vipaumbele tisa vya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27.

Vipaumbele hivyo ni pamoja na Kuimarisha uhifadhi, ulinzi, na matumizi endelevu ya rasilimali, miundombinu na kutangaza utalii, kuendeleza mazao ya utalii (MICE), Kuimarisha uzalishaji na masoko ya mazao ya misitu na nyuki, matumizi ya teknolojia za kisasa katika usimamizi wa rasilimali, ukusanyaji wa mapato, Utafiti, Ubunifu na Maendeleo ya Rasilimaliwatu, mapitio ya Sera, Sheria na Kanuni pamoja na

kuboresha mazingira ya kazi, mifumo ya usimamizi wa utendaji na uwajibikaji.

Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa mwaka wa fedha 2026/27 pamoja na mambo mengine imepanga kuendelea na ujenzi wa barabara ya Loduare Golini kwa kuanzia kipande cha kilomita 29.5 kutoka Loduare hadi Seneto (njia ya kushukia kreta ya Ngorongoro).

Ujenzi wa barabara hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa watalii kusafiri kwa raha mustarehe hasa ikiwa ni maandalizi ya kuboresha huduma kuelekea michuano ya AFCON pamoja na kufungua barabara mpya kuelekea katika vivutio vingine sambamba na uibuaji wa mazao mapya ya utalii.

Ngorongoro inatarajia kukarabati Mtandao wa barabara ulioko ndani ya hifadhi ya Ngorongoro wenye zaidi ya kilomita 600, zote ili ziendelee kupitika kwa wakati na kuongeza mtawanyiko wa wageni wanaotembelea vivutio ndani ya hifadhi