Kaimu Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha Bw. Kenneth Nindie, akizungumza na Menejimenti ya Wizara hiyo wakati wa mafunzo ya Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani. Mafunzo hayo yalihusisha Menejimenti ya Wizara ya Fedha na yalifanyika katika Hotel ya Morena mkoani Morogoro.

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA Evaristo Mwalongo, akizungumza na Menejimenti ya Wizara hiyo wakati wa mafunzo ya Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani. Mafunzo hayo yalihusisha Menejimenti ya Wizara ya Fedha na yalifanyika katika Hotel ya Morena mkoani Morogoro.

Baadhi ya Viongozi wa Idara na Vitengo vya Wizara ya Fedha wakifatilia mawasilisho mbalimbali yaliyotolewa na Wawezeshaji kutoka Kampuni ya Ushauri (KPMG) wakati wa mafunzo ya Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani wa Wizara ya Fedha, yaliyohusisha Menejimenti ya Wizara ya Fedha yaliyofanyika katika Hotel ya Morena mkoani Morogoro.

Mwezeshaji kutoka Kampuni ya Ushauri (KPMG), Bi. Peninah Musya, akifanya wasilisho wakati wa mafunzo ya Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani wa Wizara ya Fedha, yaliyohusisha Menejimenti ya Wizara ya Fedha Wizara hiyo yaliyofanyika katika Hotel ya Morena mkoani Morogoro. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Morogoro)
…………
Na. Chedaiwe Msuya, WF, Morogoro
Kaimu Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Kenneth Nindie, amewataka washiriki wa mafunzo ya Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani wa Wizara ya Fedha kuyatekeleza kwa vitendo katika majukumu yao ya kila siku.
Ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo hayo kwa Menejimenti ya Wizara yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena mkoani Morogoro.
Alisema kuwa utekelezaji wa mwongozo huo ni nguzo muhimu ya kuimarisha uwajibikaji na kuhakikisha rasilimali za umma zinasimamiwa kwa ufanisi na uwazi.
Aidha, alisisitiza kuwa udhibiti wa ndani si dhana ya nadharia pekee, bali ni mfumo unaohitaji kuishiwa kwa vitendo ili kuleta matokeo chanya katika utendaji wa taasisi.
Kwa upande wake, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA Evaristo Mwalongo, alisema kuwa mafunzo hayo yamekusudia kuwajengea washiriki uelewa mpana kuhusu wajibu wa kila mtumishi kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini, na namna bora ya kudhibiti viatarishi vinavyoweza kuathiri utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Wakizungumzia mafunzo hayo washiriki wa mafunzo hayo walieleza kuwa wamenufaika kwa kiwango kikubwa na wameahidi kuyatumia katika kuboresha ufanisi wa kazi zao.
Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo dhana ya udhibiti wa ndani, malengo yake, wajibu wa kila mtumishi kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini, na udhibiti
Kaimu Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha Bw. Kenneth Nindie, akizungumza na Menejimenti ya Wizara hiyo wakati wa mafunzo ya Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani. Mafunzo hayo yalihusisha Menejimenti ya Wizara ya Fedha na yalifanyika katika Hotel ya Morena mkoani Morogoro.
