Balozi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Dkt. Suleiman H. Suleiman amewasilisha hati ya uwakilishi kwa Mheshimiwa Bw. Hong Lei, Msaidizi Waziri na Mkugenzi Mkuu wa Idara ya Itifaki ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Wachina. Shughuli hiyo ikifanyika tarehe 14 Mei 2026 kwenye Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya China. Kabla ya hafla hiyo Balozi Suleiman na Bw. Hong Lei walifanya mazungumzo yaliyohusu zaidi kuendeleza ushirikiano wa China na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya kijamii, kidiplomasia, Uwekezaji katika Miradi mikubwa ya kimkakati na Uchumi kwa ujumla.
BALOZI SULEIMAN AZUNGUMZA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA
By fullshangwe
May 14, 2026 | 4:59 pm

Related Stories
View all
Mchanganyiko
45 minutes ago
WAZAZI WATAKIWA KUTOWAHARAKISHA WATOTO KUINGIA MAMBO YA UTU UZIMA
Meneja wa Shule hiyo , Mchg. Manase Meshorori akizungumza katika mahafali hayo jijini ArushaMwalimu Mkuu wa Shule hiyo ,Mary Mollel akizungumza katika.mahafali hayo Happy…
Mchanganyiko
1 hour ago
RWEZIMULA AZINDUA NYUMBA ZA MAKAZI CHUO CHA MAGEREZA KIWIRA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Franklin Jasson Rwezimula, akizungumza na mafundi walioshiriki ujenzi wa nyumba mpya za…