Wataalam kutoka Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) wametembelea Kiwanda kikubwa Cha Insignia Ltd kilichopo Kata ya Kibada katika Manispaa ya Kigamboni jijini Dar Es salaam .

Kiwanda hicho kinazalisha vifungashio vya plastiki vya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na ndoo za rangi ,makopo ya rangi pamoja na vifuniko vya vinywaji baridi.

Wataalam hao walipokelewa na ndugu. Edson Lukula ambaye ni mkuu wa Idara ya utawala na lasilimali watu.

Ziara hiyo ilijumuhisha wataalam kutoka idara na vitengo mbali mbali kama Masoko, Maabara, Nishati ,Kitengo Cha Chakula pamoja na Mazingira .

Wataalam hao walitembelea maeneo mbali mbali ya kiwanda ambapo waliona namna ambavyo Kampuni hiyo inaweza kushirikiana na TIRDO katika kupiga hatua ikiwa ni katika maeneo ya ukaguzi na usimamizi wa Nishati pamoja na Mazingira.

Wataalam walioshiriki ziara ni Dr Gurdeep Jaswat Hunjan Kutoka Kitengo Cha Chakula na Bioteknolojia ,ndugu Burhan Mdoe Daud (Afisa Masoko ), Mhandisi Raymond Mfanga (Mtaalam wa nishati), Justine Kitabaganda Tryphone (Maabara ya Kemia ) , Kennan Justin( Maabara ya Ngozi ) pamoja na ndugu Isaya Mtimila kutoka Idara ya TEHAMA.

Kiwanda kimetoa ajira Kwa watu zaidi 300 walioajiriwa Moja Kwa Moja nakuwawezesha wataazania kupata fursa ya ajira .

Uongozi wa Insignia co ltd umeshukuru kupata nafasi yakutembelewa na wataalam wa TIRDO nakuahidi kuendelea kushirikiana na TIRDO katika eneo la ukaguzi wa matumizi bora ya nishati. uongozi umeushukuru TIRDO kwa kufanikisha ziara hiyo na Kisha kutoa ushauri wa awali wa kitaalam ili kuanza safari ya kwenda hatua ya pili ya ushirikiano kupata fursa ya kazi kubwa zaidi za kitaalam Viwandani.