Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa leo, Mei 6, 2026, kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Simba SC ilipata bao kupitia kwa Clatous Chama kipindi cha pili na kufikisha pointi 43, wakiwa nafasi ya pili katika msimamo wa ligi. Huku JKT Tanzania, baada ya kupoteza mchezo huo, wanabaki na pointi 32 katika msimamo wa ligi.
