Dakika chache baada ya Yanga kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC, uongozi wa timu hiyo leo Jumatano, Mei 6, 2026 umetangaza kumfuta kazi Kocha Mkuu wa timu hiyo, Pedro Goncalves raia wa Ureno.

Taarifa ya Yanga imeeleza kuwa benchi la ufundi la timu hiyo litakuwa chini ya Abdihamid Moalin hadi mwishoni mwa msimu.

“Uongozi wa Klabu ya Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu umma kuwa umemfuta kazi Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Pedro Gonçalves.