Kulikuwa na mshangao mkubwa katika soko la mjini Dodoma baada ya mwanamke mmoja kugundulika akijifanya mjamzito kwa kutumia mto ili kuwalaghai watu na kujipatia fedha kwa njia ya huruma. Tukio hilo liligeuka kuwa fedheha kubwa baada ya ukweli kufichuka hadharani.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mwanamke huyo alikuwa akizunguka sokoni akilia na kuomba msaada, akidai kuwa ana mimba kubwa na hana uwezo wa kujikimu. Watu wengi waliguswa na hali yake na kumpa fedha na msaada wa vitu mbalimbali.

Hata hivyo, baadhi ya wafanyabiashara walianza kuwa na shaka baada ya kuona hali yake haibadiliki kwa muda mrefu. Siku moja, alipojaribu kukimbia baada ya kuulizwa maswali mengi, alijikwaa na kuanguka. Ndipo mto aliokuwa ameufunga tumboni ulipojitokeza wazi mbele ya watu…. SOMA ZAIDI