
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto wakishuhudia utiaji saini wa Mikataba nane ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Kenya katika sekta mbalimbali kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 04 Mei, 2026.
Mikataba nane iliyosainiwa ni kuhusu masuala ya usimamizi wa Reli, upembuzi yakinifu wa mradi wa bomba la Gesi kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa, usaidizi wa Kisheria kuhusu masuala ya jinai, masuala ya Kilimo, utambuzi wa vyeti vya Mabaharia, usimamizi wa sekta ya Usafiri kwa njia ya maji, masuala ya Viwango pamoja na kujengeana uwezo kwenye masuala ya Utumishi wa Umma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 04 Mei, 2026.
