Na Farida Mangube Morogoro
Kemikali inayodaiwa kuwa ni sulphur imemwagika baaaa ya gari yenye namba za usajili T196 EMU mali ya kampuni ya Alhushum lililokuwa libeba kemikali hiyo kuacha njia na kugonga miti barabara kuu ya Morogoro–Iringa, karibu kabisa na Bwawa la Mindu.
Fullushangwe Blog imefika eneo la tukio na kushuhudia jitihada za dharura zikifanyika kuzuia kemikali hiyo isiingie kwenye bwawa la Mindu iwapo Mvua ikinyesha na kuhatarisha maisha ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro ambao asilimia 75 wanategemea maji safi na Salama kutoka kwenye bwawa hilo.
Mamlaka mbalimbali zimefika Katika eneo hilo zikiwemo NEMC, Bonde la Wami-Ruvu, MORUWASA na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji zikiratibu operesheni ya kudhibiti hali hiyo. Hata hivyo, wataalamu kutoka mamlaka hizo wamekataa kuzungumzia tukio hilo kwa kina wakieleza kuwa kipaumbele chao kwa sasa ni kuokoa hali.
Kwa upande wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Kati imesema wataalamu wake wako njiani kutoka Dodoma na watazungumzia tukio hilo baada ya kufika eneo husika.
Hadi majira ya saa Moja na nusu usiku mwandishi wa Fullushangwe blog anaondoka Katika eneo la tukio Bado jitihada za kuzuia kemikali hiyo isiingie kwenye mitaro inayotiririsha maji kuelekea bwawani zilikuwa zinaendelea, awali zikihusisha nguvu kazi ya watu kabla ya kuwasili kwa mitambo maalum kusaidia kazi hiyo.





