
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kushiriki katika Hafla ya Usiku wa Mtanzania ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano. Tarehe 26 Aprili 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Masauni, Waziri wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili ya Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe. Hamza Hassan Juma, pamoja na Viongozi mbalimbali wakishiriki Hafla ya Usiku wa Mtanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano. Tarehe 26 Aprili 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akitoa salamu wakati wa Hafla ya Usiku wa Mtanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano. Tarehe 26 Aprili 2026.

Washiriki mbalimbali wa hafla ya Usiku wa Mtanzania wakitoa burudani katika tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano. Tarehe 26 Aprili 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akimkabidhi cheti cha shukrani, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Dkt. Immaculate Sware Semesi, wakati wa Hafla ya Usiku wa Mtanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano. Tarehe 26 Aprili 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Hafla ya Usiku wa Mtanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano. Tarehe 26 Aprili 2026.
……………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesisitiza umuhimu wa mshikamano wa Kitaifa ikiwa ni namna muhimu ya kuwaenzi waasisi wa Muungano, Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume.
Makamu wa Rais amesema ametoa msisitizo huo, wakati wa Tamasha la Usiku wa Mtanzania ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano, lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Amesema ni msisitizo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vijana na watanzania kwa ujumla kuhusu kuwa na mshikamano kulinda umoja na amani.
Makamu wa Rais amewasihi watanzania kutafakari na kujielekeza katika kujenga mshikamano ni kuhakikisha Muungano unalindwa.
Amesisitiza umuhimu wa kuvumiliana katika utoaji wa mawazo,kushauriana kujenga utaratibu wa kukubaliana hata katika masuala yanayotoafutiana mawazo.
Awali akitoa neno la utangulizi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Tamasha hilo hilo linalenga amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano.
Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kufanikisha kutatuliwa hoja 22 kati ya 25 za Muungano. Pia amempongeza Makamu wa Rais, kwa kuongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja na kufanikisha kutatuliwa kwa hoja ya uingizaji sukari katika soko la Tanzania Bara hivyo kuufanya Muungano kuwa imara zaidi.
Aidha, amesema shughuli mbalimbali zimefanyika katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano, zikiwemo uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo, makongamano na mjidala kuhusu Muungano ikilenga kutoa elimu kwa wananchi.
Aidha Serikali zote mbili kupitia vyama vya michezo zimeshirikiana katika kuandaa mashindano ya mpira wa miguu ya Kombe la Muungano yanayoendelea Zanzibar. Ameongeza kwamba, elimu ya Muungano itatolewa pia katika Msafara wa Muungano (Muungano Caravan) ambao utazinduliwa Mei 03, 2026 jijini Dar es Salaam na kuhusisha wilaya zote.




