Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akizindua gari tayari kwa kuwakabidhi TANESCO
Na. Mwandishi wetu, Katavi
Shirika la umeme (TANESCO) wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi limepokea gari moja aina ya toyota crane kwa ajili ya kuwawezesha kufanya kazi kwa urahisi na hivyo kuondoa changamoto ya mafundi wa shirika hilo kubeba nguzo za zege kwa mikono wakati wa kubadilisha nguzo na kufikisha umeme katika maeneo yasiyo na huduma hiyo.
Wakizungumzia changamoto walizopitia awali kutokana na kukosa gari viongozi wa TANESCO akiwemo mhandoso Yoram Mteni ambaye ni kaimu meneja wa mkoa na Kaimu meneja wa wilaya ya Tanganyika Adam Ali walisema wakati mwingine walitakiwa kwenda kwa haraka kubadilisha nguzo lakini walichukua muda mrefu kutokana na kukosa gari lenye uwezo huo.
Pia wameishukuru serikali ya awamu ya sita ya mama DK. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea gari hilo.
Akikabidhi gari hilo mkuu wa wilaya ya Tanganyika bwana Onesmo Buswelu ametaka gari hilo litumike ipasavyo na kutunzwa vizuri kwa manufaa ya watu wa Tanganyika.
Naye mmoja wa mafundi wa TANESCO Sadick Mohamed amesema mtambo huo utawarahisishia kazi.




