Kaimu Katibu Mkuu wa ALAT ,Thomas Vungwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao hicho jijini Arusha
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha.JUMUIYA ya Tawala za mitaa Tanzania (ALAT) imetangaza rasmi uchaguzi wa viongozi wa ALAT -Taifa utakaofanyika april 22 -23 ,2026 katika ukumbi wa mikutano wa AICC uliopo jijini Arusha .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Kaimu Katibu Mkuu wa ALAT ,Thomas Vungwa amesema kuwa uchaguzi huo unafanywa kwa ngazi ya Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti,Wajumbe wa Kamati ya utendaji,Mwenyekiti wa WASEMI,Makamu Mwenyekiti wa WASEMI ,pamoja na Kamati tendaji ya WASEMI.
“Kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha katiba ya ALAT (2014) pamoja na kanuni za kudumu za mikutano na uchaguzi wa viongozi wa ALAT za mwaka 2009 (kanuni ya 27,28,29,30,31,32,33,na 34 natoa rasmi tangazo la kuitishwa kwa uchaguzi wa viongozi wa jumuiya “amesema Vungwa .
Amesema kuwa,uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa ALAT katika ngazi ya Taifa unazingatia kifungu cha 10 cha Katiba ya ALAT ambacho kinaelekeza uchaguzi wa viongozi wa jumuiya (Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti )utafanywa kwa waombaji kujaza fomu za maombi kuwania nafasi hizo .
“Mwombaji ataungwa mkono na wajumbe wawili kutoka kila kanda ambapo fomu zitachukuliwa kuanzia april 17 hadi april 21 ,2026 na fomu za maombi zitawasilishwa kwenye ofisi ya sekretariet ya jumuiya kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana april 21 ,2026 katika ukumbi wa kimataifa wa AICC uliopo mjini hapa.’amesema .
Amefafanua kuwa zoezi la kichuja wagombea litafanyika april 21 ,ambapo zoezi la wagombea kujinadi na uchaguzi litafanyika april 22,2026.
Aidha akitaja wajibu wa mgombea amesema kuwa kwa wale wanaokusudia kugombea nafasi hizo wanapaswa kuzingatia na kutimiza taratibu zote zilizoelekezwa katika kanuni na mwongozo uliotumwa kwa makatibu na wenyeviti wa matawi ya ALAT Mikoa .
Vungwa amesema kuwa,ALAT imekuwa ikifanya uchaguzi wa viongozi wake kila baada ya miaka mitano .
Aidha ametoa wito kwa wale wote wenye nia ya kugombea nafasi hizo kutumia fursa hiyo huku wakifuata miongozo na kanuni zilizowekwa .





