Mkuu wa wilaya ya ilala mhe Sophia Mjema akimkaribisha Naibu waziri OR Tamisemi Na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe Mwita Waitara kuongea na wadau wa Barabara walioudhulia katika makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa Barabara na madaraja ya Ulongoni A na B.
Mstahiki meya manispaa ya ilala mhe Omar kumbilamoto akizungumza katika makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa Barabara na madaraja.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ndg Jumanne shauli akitoa taarifa juu ya mradi wa ujenzi wa Barabara km 7.5 pamoja na madaraja ya Ulongoni B na A (zimbili).
**************************
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala wamekabidhi ujenzi wa madaraja matatu Jimbo la Ukonga kwa wakandarasi.
Madaraja hayo yaliokabidhia jimboni humo daraja la Zimbili, Ulongoni A na Ulongoni B ambapo kazi za ujenzi zinatarajia kuanza Aprili Mosi mwaka huu.
Utekelezaji wa mradi huo wa unafanywa na DMDP sambamba na ujenzi wa barabara za kiwango cha lami.
Akizungumza katika makabidhiano hayo katika ukumbi wa Arnatogluo Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam leo Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Mhe.Mwita Waitara Mbunge wa Ukonga (CCM) aliwataka Wananchi waache malumbano katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali badala yake waache Wakandarasi watimize wajibu wao.
Aidha, Mhe.Waitara alitaka mikataba ya masharti ya ujenzi yazingatiwe waache wakandarasi watimize wajibu wao ili kuteleza miradi kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala Bw.Jumanne Shauri, alisema manispaa hiyo inatekeleza miradi ya DMDP kwa fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia ujenzi utakaoghalimu shilingi za Kitanzania bilioni 115.
“Moja ya miradi inayotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa madaraja makubwa mawili ambayo ni daraja la ulongoni B litakalo jengwa pamoja na Barabara kiwango cha lami Kilomita 7.5 na daraja la Zimbili Ulongoni A”alisema Bw.Shauri.
Mkurugenzi Shauri alisema ujenzi wa daraja la Ulongoni B na barabara kilomita 7.5 kitajengwa na stendi ya Kinyelezi ya kisasa na Mkandarasi M/s China Railway Seventh Gruop kwa gharama za shilingi 17,608,000,955.08.
Aidha Bw.Shauri alisema daraja la Zimbili Ulongoni A litajengwa na Mkandarasi wa M/s Chongqing Internationl Construction Corporation kwa gharama za shilingi 4,304,066,255.20 ujenzi wake utakamilika ndani ya miezi kumi tangu kuanza kwa ujenzi wake madaraja yote yapo mto Msimbazi.
Nae Mkuu wa Wilaya Ilala Dkt. Sophia Mjema alisema amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mkandarasi aliyepewa tenda ya ujenzi mpaka ujenzi utakapoisha endapo zikitokea changamoto katika ujenzi huo watoe taarifa Mamlaka husika kwa kufuata utaratibu.
“Awali eneo hilo la Ulongoni A na Ulongoni B kulikuwa na changamoto kubwa kutokana na kukosekana kwa mawasiliano kwa juhudi za Rais wetu John Magufuli sasa serikali yetu pendwa ya awamu ya tano fedha zimepatikana sasa ujenzi wake unaanza rasmi naomba wananchi tuunge mkono juhudi za Rais ” alisema Dkt.Mjema.
Naye Meya wa halmashauri ya manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto alipongeza serikali na kuwataka wakandarasi kumaliza ujenzi ili wananchi wa Jimbo la Ukonga wanaotumia vivuko hivyo kuwaondolea adha inayokuwa wakipata kila wakati wa mvua kwa kukosa mawasiliano.