Afisa habari wa TRA United ,Christina Mwagala akizungumza kuhusu mechi hiyo kesho jijini Arusha .

Happy Lazaro,Arusha

Arusha .TIMU ya TRA Sports Club yatamba kuifunga Simba Sports Club kwenye mchezo wa kukata na shoka utakaofanyika kesho katika.uwanja wa mpira wa Stadium jijini Arusha.

Akizungumzia kuhusu mechi hiyo ya kukata na shoka ,Afisa habari wa TRA United ,Christina Mwagala,amesema kuwa kesho kuna mechi ya ligi kuu NBC kutoka Tanzania bara ambapo TRA sports Club inamkaribisha Simba sports Club na maandalizi yameshakamilika .

Akizungumza kuhusu mechi hiyo ya kukata na shoka amesema kuwa, hawajawahi kupoteza mchezo hata mmoja na wanaahidi kufanya vizuri zaidi kwenye mchezo huu.

“Sisi tuna uhakika kesho Simba anafukuzwa kesho wanaArusha tukiamka tunaomba Mungu mvua isinyeshe na hata ikinyesha ya mawe kesho TRA tunacheza .”amesema Christina .Ameongeza kuwa,kiingilio ni Tsh 50,000 VIP ,Tsh 30,000 VIP A na B na shs 10,000 mzunguko .

Aidha amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mechi hiyo kuja kujionea mchezo huo kabambe .