Na. Meleka Kulwa- Fullshangwe Blog, Dodoma 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema  kifo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Vangimembe Lukuvi, kimeacha simanzi na butwaa kubwa kwa Watanzania wengi.

Amesema kuwa alikuwa akiwasiliana na Mheshimiwa Lukuvi mara kwa mara na kushauriana naye kuhusu masuala mbalimbali ya kazi hadi muda mfupi kabla ya kupokea taarifa za kubadilika kwa hali yake ya afya, huku wakiwa wanaendelea kupanga shughuli za Serikali na masuala ya Bunge.

ameyabainisha hayo  Machi 27, 2026 Jijini Dodoma wakati alipokuwa ameongoza waombolezaji kwenye kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) ambaye pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Isimani Mhe. William Vangimembe Lukuvi.

Aidha amebainisha kuwa Lukuvi alikuwa na uwezo mkubwa wa uratibu na alihakikisha shughuli za Serikali zinaendelea kwa ufanisi, akieleza kuwa hata alipokuwa kwenye ziara ndefu, hakukuwa na pengo katika maandalizi ya Bunge na kamati kwa kuwa marehemu aliendelea kusimamia majukumu hayo kikamilifu.

Pia ameongeza kuwa marehemu alikuwa na busara, ukomavu wa kisiasa na weledi mkubwa wa kazi, huku akiwa mlezi na mwalimu kwa wabunge na mawaziri wengi kwa kuwapa ushauri uliosaidia kuboresha utendaji wao.

Amesema kuwa Lukuvi alikuwa kiungo muhimu katika kuimarisha mahusiano kati ya Serikali na Bunge, hasa katika nyakati ambazo kulikuwa na changamoto za hoja na mijadala, akihakikisha pande hizo zinaendelea kushirikiana kwa ufanisi.

Aidha amebainisha kuwa alikuwa na uwezo wa kuelezea masuala ya kazi kwa lugha rahisi kwa wizara mbalimbali, jambo lililosaidia kuongeza ufanisi wa ushirikiano ndani ya Serikali.

Pia ameongeza kuwa marehemu alikuwa na kiwango cha juu cha kujitolea, nidhamu binafsi ya kazi na uzalendo, sifa zilizomfanya kuaminiwa na Mheshimiwa Rais katika majukumu ya uratibu.

Aidha, Amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuwa bega kwa bega na familia ya marehemu kufuatia maelekezo ya Mheshimiwa Rais, huku akitoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na Watanzania wote walioguswa na msiba huo.

Pia, ameelezakuwa licha ya majonzi, mafunzo yaliyotolewa wakati wa ibada yamekuwa faraja kwa waombolezaji kwa kuwakumbusha umuhimu wa ubinadamu na mshikamano. Akisema kuwa 

” Mungu ndiye mwanzilishi na mwisho wa maisha ya kila mmoja, hivyo naiombea familia kuwa na moyo wa ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu” amesema Dkt. Nchemba 

Awali akizungumzaNaibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratıbu na Wenye Ulemavu), Ummy Nderiananga, amesema kuwa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratıbu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi, alikuwa ni mtu aliyetanguliza mbele kazi na maslahi ya taifa, vitu ambavyo wao kama watendaji waliokuwa chini yake wamebaki navyo. 

‎Aidha, amebainisha kuwa Lukuvi atabaki kuwa mwalimu mwema, mlezi mahiri ambaye pamoja na kumfunza kazi bado alimfunza na maisha.